Polisi
nchini Ujerumani wamemuomba radhi mtu mwenye mkono mmoja aliyepigwa
faini kwa kuendesha baiskeli yenye breki moja badala ya mbili kama
inavyotakiwa kisheria. Miezi mitatu baada ya Bodgan Ionescu kupigwa
faini ya Euro 25, polisi wa mjini Cologne wamerejesha fedha hizo
wakisema walivuka mipaka. Bwana Ionescu ameyaambia magazeti kuwa amehisi
kubaguliwa kutokana na ulemavu wake lakini ameshukuru suala hili sasa
limekwisha.
0 comments:
Post a Comment