Facebook

Thursday, 17 July 2014

Serikali na Waasi wabadilishana wafungwa Mali.

 Photo: SERIKALI NA WAASI WABADILISHANA WAFUNGWA MALI
Serikali ya Mali na waasi wa Tuareg wamebadilishana wafungwa kama ishara ya wema kabla ya kuanza mazungumzo ya amani.
Jeshi limesema wanajeshi 45 waliokuwa wakishikiliwa na waasi kaskazini mwa nchi hiyo waliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bamako.
Waasi 41 wa Tuareg waliokuwa wakishikiliwa Bamako nao walipakizwa ndani ya ndege iliyowaleta wanajeshi hao na kuelekea kaskazini.
Hatua hii inakuja kabla ya mazungumzo ya amani yanayotarajiwa kuanza katika mji mkuu wa Algeria, Algiers. Pande hizo mbili zilikubaliana kusitisha mapigano mwezi Mei.
Makundi ya waasi- likiwemo la MNLA - yalichukua udhibiti we eneo kubwa la Kaskazini mwa Mali katika miezi ya hivi karibuni.
Mwaka 2012 uasi wa Tuareg kaskazini mwa Mali ulisababisha mapinduzi ya kijeshi mjini Bamako na udhibiti wa waasi upande wa kaskazini.
Utawala wa kiraia ulirejeshwa tena mwaka 2013, lakini waasi bado wamesalia katika baadhi ya maeneo.
Serikali imetuhumu waasi wa Tuareg - kuwa wanaungwa mkono na wapiganaji wa al-Qaeda.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment