Zaidi ya karatasi elfu moja za kura za uchaguzi uliokuwa na utata wa
Malawi, zimeteketezwa na moto katika mazingira ya kutatanisha. Chama cha
upinzani cha MCP kilitaka kura hizo zihesabiwe upya za kiti
cha ubunge katika jimbo moja la mjini Lilongwe.
Wananchi wengi wa
Malawi wanashuku uchaguzi wa mwezi Mei, ambao Peter Mutharika alimshinda
Joyce Banda, ulivurugwa. Waandishi wa habari wanasema iwapo kura hizo
zingehesabiwa na kubadili matokeo rasmi, huenda matokeo ya uchaguzi wote
yangetiliwa mashaka.
0 comments:
Post a Comment