Facebook

Saturday 21 March 2015

'HOUSE GIRL' ASABABISHA KIFO, VIJANA WA KAMASAI "MORANI" WACHOMA NYUMBA KULIPIZA KISASI ARUSHA

Makundi ya vijana wanaosadikiwa kuwa ni wa jamii ya kimaasai
maarufu kama “Morani” katika eneo la Olasiti Jijini Arusha,
wameteketeza kwa moto mali mbalimbali zikiwemo nyumba pamoja na
magari ya wakazi wawili wa eneo hilo, wanaotuhumiwa kumpiga na
kumsababishia kifo kijana mmoja wa jamii hiyo.
Kijana Melita John anadaiwa kuuawa na Bernard Kavishe mkazi wa
Olasiti akishirikiana na majirani zake wawili akimtuhumu kijana huyo
kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msichana wake wa kazi za ndani
ambaye ni binti wa miaka 17 anayefahamika kwa jina la Monica
Emanuel.

Taarifa zaidi zinadai kuwa hatua ya morani wa kimaasai kujichukulia
sheria mkononi na kuteketeza nyumba na magari pamoja na mali
nyingine za watuhumiwa hao ni katika kulipiza kisasi kutokana na kifo
cha mwenzao wanayedai hakuwa na hatia.
Inadaiwa mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji hayo Benard Kavishe
baada ya kuwasili nyumbani kwake majira ya saa saba mchana na
kugonga gate la nyumbani kwake ilimchukua muda wa dakika kumi
msichana wake wa kazi kufungua ndipo alipoingia ndani na kumkuta
kijana Melita akiwa bila nguo ndipo alipowaita majirani wenzake na
kumshambulia kwa kipigo hadi kumsababishia mauti
Jeshi la Polisi kupitia wa Kaimu kamanda wa Mkoa wa Arusha
Kamishna Msaidizi Edward Balele akithibitisha tukio hilo amesema
baada ya watuhumiwa wanaosadikiwa kushiriki katika mauaji ya
kijana Melita wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi..

0 comments:

Post a Comment