Mshukiwa mmoja wa ubakaji
aliyekuwa miongoni mwa genge la watu waliombaka msichana mmoja kwa Jina
Liz mwaka jana ,na kumtupa ndani ya shimo, amefikishwa mahakamani leo.
Mshukiwa huyo alikuwa mmoja wa watuhumiwa ambao
polisi waliwapa adhabu ya kukata nyasi kwa kitendo cha ubakaji na kisha
kuachiliwa.Washukiwa wengine watano hawajulikani waliko.Kesi ya Liz ilisababisha ghadhabu sana sio Kenya tu bali duniani kote hasa kwa ambavyo polisi waliishughulikia.
Mnamo Jumatatu mamia ya wanawake waliandamana mjini Busia ambako kesi hiyo inafanyika wakiunga mkono haki kwa Liz huku kesi hiyo ikianza kusikilizwa.
Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopinga dhuluma dhidi ya wanawake, uliongoza waandamanaji ambao baadaye walikusanyika katika kituo cha mkuu wa jimbo, Isaiah Nakoru.
Waliotia saini nyaraka hizo wanamtaka mkuu wa polisi kuwakamata washukiwa na kitendo hicho cha unyama dhidi ya Liz ambao walimbaka na kisha kutupa mwili wake ndani ya shimo lenye urefu wa futi 25 mjini humo.
Viongozi wa maandamano wanasema kuwa idadi kubwa ya wasichana waliobakwa tangu kusikika kwa kisa cha Liz wamekuwa wakienda kuwashitaki watuhumiwa kwa polisi.
Liz alibakwa na wanaume sita ambao walimuwacha na majeraha mabaya kwenye mwili wake kiasi cha kulazwa hospitalini kwa miezi kadhaa.
Mamake Liz alikuwa miongoni mwa waandamanaji.
0 comments:
Post a Comment