Facebook

Thursday, 10 July 2014

Tundu Lissu: ‘Tunataka kuziona mashine za BVR’

 Mhe.Tundu Lissu

Mabishano makali yameibuka kwa viongozi wa vyama vya upinzani juu ya kuanzishwa kwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambalo litatumia mfumo mpya wa BVR.
Mabishano hayo yameanza kwa Mbunge wa Singida Tundu Lissu kutaka kuoneshwa mashine ambazo zitatumika katika mchakato wa kuandikisha wapigakura pamoja na kuwekwa wazi kampuni ambayo zimetoka mashine hizo.
“Mwenyekiti tunataka kuziona kwa umakini mkubwa mashine hizo za BVR ambazo zitatumika kwenye kuandikisha wapiga kura na kama mashine hiyo haijaandaliwa vya kutosha kuweza kuiona wawakilishi wa vyama za siasa basi tuendelee na mada nyingine ya kutoa maona ya mchakato huo, lakini sio kujadili hiyo mashine ambayo hatujaijua utendaji wake wa kazi”, alisema Lissu.
Kwa upande wake Dr. Slaa naye alimuunga mkono Tundu Lissu kwa kusema kuwa, vitu hivi havitakiwi kwenda kiharaka na mashine hiyo haiwezi kujadiliwa na kutoa mawazo jinsi gani ya kutumia mashine hiyo, kama haiwezekani basi kipangwe kikao kingine cha kuikagua hiyo mashine mpya ya kuandikisha wapigakura.
Aidha Tundu Lissu aliongeza kuwa itakuwa ngumu kukamilisha zoezi hilo kwa siku 19 kwa sababu vitambulisho vya mkazi mpaka sasa vinasuasua ukamilifu wake na unazaidi ya miaka miwili toka umeanza.
Profesa Ibrahim Lipumba yeye kwa upande ake alisema kuwa, Rais Dr. Jakaya Kikwete anatakiwa awaambie wananchi juu ya kuanzishwa kwa daftari hilo, kwa sababu yeye aliwaambiwa wananchi kuwa vitambulisho vya mkazi ndio vitatumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, sasa imekuaje amekuja na kitu kipya kabla ya kile cha zamani hatujajua mapungufu yake, hatujajua mpaka sasa watu wangapi wameandikishwa.
Mtaalamu huyo wa uchumi duniani aliongeza kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma pamoja na kupotezeana muda wa kuzalisha na kukuza kipato cha mtanzania, bajeti iliyopita hivi karibuni inaonesha kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepangiwa Bilioni 8 tu za matumizi, sasa leo tunaambiwa kuna hilo Daftari ambalo litatumia Bilioni 200, fedha hizo zimetoka wapi? kwanini pesa hizo wasizitumie kwa maendeleo ya watanzania? wanazitumia ndivyo sivyo.
Kwa upande wake Kinana alisema kuwa, kila kipya kinachoanza kinakuwa na changamoto zake lakini mradi huo ni mzuri utaweza kuwasaidia kupunguza migogoro kipindi cha uchaguzi.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment