Facebook

Thursday, 10 July 2014

Juventus yathibitisha kumuwania Patrice Evra.

Photo: JUVENTUS YATHIBITISHA KUMUWANIA PATRICE EVRA

BBC Sport pamoja na vyombo vingi vya habari vimetoa habari kuhusu uthibitisho wa klabu ya Juventus kumtaka Patrice Evra. Juventus wamewasiliana na uongozi wa United na kutoa kiasi kinachosemekana kuwa kati ya Pound mil 1.2 mpaka Pound mil 2. 

Patrice Evra mwenye umri wa miaka 33 amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 45 katika mashindano yote msimu uliopita. Evra alikua miongoni mwa wachezaji walioiwakilisha timu ya taifa ya Ufaransa kwa mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka huu na kufanikiwa kucheza michezo minne kati ya mitano kwa hatua waliyofikia. 

Alijiunga mwezi January mwaka 2006 akitokea klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa kwa ada ya Pound mil 5. Amefanikwa kucheza michezo 379 akishinda mara 5 ubingwa wa ligi kuu ya uingereza na ubingwa wa ulaya mwaka 2008. 

Patrice Evra anaonekana atajiunga na mabingwa hao wa serie A baada ya taarifa kudai wamemuandalia mkataba mnono wa miaka miwili licha ya kuwa tayari Manchester United wameshamrefushia mkataba wa mwaka mmoja. 

=/ D.P /=

0 comments:

Post a Comment