Facebook

Tuesday, 17 June 2014

Wahadhiri wa Udom wadaiwa kufanya mgomo baridi

Chuo Kikuu cha Dodoma ndio chuo kikubwa nchini Tanzania Chuo hicho kipo mkoani Dodoma, makao makuu ya nchi ya Tanzania.
Chuo Kikuu cha Dodoma ndio chuo kikubwa nchini Tanzania Chuo hicho kipo mkoani Dodoma, makao makuu ya nchi ya Tanzania.
Taarifa zinasema wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma wamefanya kikao cha siri leo asubuhi na kutoingia madarasani kuelekea kuanza kusimamia mitihani (University Examinations) ya kumaliza muhula wa pili wa masomo.

Taarifa News imeongea na mwanafunzi wa shahada ya sheria chuoni hapo ambaye alidai kuwa, walikuwa waanze kufanya mitihani leo ila cha kushangaza hakuna mwalimu aliyekuja kwenye chumba hicho zaidi ya afisa utawala wa chuo ambaye alikuja kuwaambia kuwa wahadhiri wanadai kuna mambo hayajakaa sawa na hivyo waendelee kukaa karibu na vituo vyao ya kufanyia mitihani.
Chanzo cha mgomo hakijatajwa japo kinasemekana kuhusiana na masuala ya fedha
“Kwa kweli hatujui nini kimesababisha walimu hawa kutoingia madarasani, japo kuna fununu kuwa ni kuhusiana na masuala ya pesa”, alieleza mwanafunzi huyo.
“Hatujui kuwa mgomo huo baridi utaisha lini”, aliongeza.
Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:

Post a Comment