Usafiri wa umma nchini Kenya utaanza kutumia mfumo wa kisasa wa kulipa nauli kwa njia ya elektroniki.
Kuanzia sasa, matatu zinazotumiwa na wananchi wengi, zitalazimika kuanza kutumia mfumo huo mpya. Siku ya Jumanne (leo) ilikuwa siku ya mwisho kwa watu kulipa nauli kwa fedha taslimu, lakini mamlaka ya usafiri imesema shughuli hiyo itaendelea kufanywa taratibu.

Mfumo huo utakuwa ukifanana na mfumo unaotumika jijini London, nchini
Uingereza ambapo hutumia kadi zijulikanazo kama Oyster. Wateja hulipa
fedha katika wakala maalum, au kutumia M-pesa au mfumo wowote wa simu,
na fedha hizo huingizwa katika kadi hiyo maalum ya kulipia
kieleketroniki.
Mamlaka ya usafiri na usalama ya taifa ya Kenya (NTSA)
imesema inadhani hatua hiyo itapunguza rushwa na kuongeza mapato.
Wamiliki wa matatu pia wamesema wameona faida za mfumo huo.
0 comments:
Post a Comment