Facebook

Sunday, 6 July 2014

Dereva asiye na mikono azuiwa kuendesha gari China.

DEREVA ASIYE NA MIKONO AKATAZWA KUENDESHA GARI
Salim Kikeke's photo.
Polisi nchini China wamemkamata mtu asiyekuwa na mikono akiendesha gari. 
 Salim Kikeke's photo.
Bwana huyo Wo Guo (45) si tu kwamba hakuwa na leseni bali alikuwa akitumia mguu wake wa kulia kubadili gia huku mguu wa kushoto ukikanyaga mafuta na breki.

Salim Kikeke's photo. 
 
Msemaji wa polisi amesema: "Ni jambo la ajabu, lakini ni hatari sana kwake kuendesha gari." Polisi huyo amesema itakuwa vyema kama ataajiri dereva wa kumuendesha. Gari la bwana Wo linashikiliwa na polisi ili kumzuia asiendelee kuendesha.
Picha na taarifa kutoka Metro na CEN.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment