Kapteni huyo wa Selecao alifunga bao la kwanza katika mechi ya robo fainali dhidi ya Colombia kabla ya kupewa kadi ya pili ya njano,jambo linalomfanya ashindwe kucheza mechi inayofata dhidi ya Ujerumani.
Nyota wa Selecao Neymar atakosa mechi zote zilizobaki baada ya kupata maumivu makali ya mgongo katika mechi iliyopigwa siku ya Ijumaa,lakini Mourinho anaamini kuwa Brazil wanapaswa kuhuzunika baada ya kumkosa Thiago Silva zaidi ya Neymar kwa sababu pengo la mlinzi huyo nivigumu kuliziba.
Aliendelea kutoa maoni yake katika gazeti maarufu la michezo la Hispania Marca,kwa kusisitiza kuwa Brazil wanamhitaji Neymar kwa sababu ni hodari akiwa uso kwa uso na mlinda mlango,pia anaweza akacheza vizuri mipira ya adhabu nakueza kufunga kwa umahiri mzuri.
Hatahivyo amedaikuwa anaamini kuwa mchezaji wa Napoli Henrique anaweza akaziba pengo lililoachwa na Neymar,huku Dante akicheza nafasi iliyoachwa wazi na Thiago ambapo atachuana na wachezaji wengi aliozoea kucheza nao akiwa katika timu ya Bayern Munich,pamoja na wachezaji wengine wa Bundesliga.
0 comments:
Post a Comment