Aliyekuwa mshabuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa, 25, amekamilisha
usajili wake kwenda Chelsea na kusaini mkataba wa miaka mitano. Ada ya
uhamisho inadhaniwa kuwa takriban pauni milioni 32.
"Nimefurahi sana kusaini Cheslea," amesema Costa. "Kila mtu anafahamu ni klabu kubwa katika ligi yenye ushindani, na nina hamasa kubwa ya kuanza kucheza England."
Costa anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Chelsea, baada ya Cesc Fabregas na Mario Pasalic.
Costa alifunga magoli 36 katika mechi 52 alipokuwa Atletico msimu uliopita, na kuiwezesha kushinda kombe la La Liga kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996 na pia kufika fainali ya Champions League.

0 comments:
Post a Comment