Facebook

Saturday, 12 July 2014

Israel Kuendeleza Mashambulizi Gaza.


Israel imesema kuwa itaendeleza
mashambulizi yake katika ukanda wa Gaza
hadi pale kundi la wapiganaji wa Hamas
litakapositisha kurusha makombora katika
maeneo ya taifa hilo.
Waziri mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu
amesema kuwa hakuna shinikizo zozote za
kimataifa zitakazozuia taifa lake kutumia uwezo
wake na kwa matamshi yake mwenyewe
akasema kuwa hakuna shambulizi lolote la
kigaidi katika Gaza lenye kinga.
Zaidi ya watu 110 wengi wao wakiwa raia wa
Palestina wameuawa kufuatia mashambulizi ya
siku nne yanayotekelezwa na Israel katika eneo
la Gaza.
Alipoulizwa iwapo Israel ilikuwa inajiandaa
kutuma jeshi la ardhini nchini Palestina ,bwana
Netanyahu alijibu kuwa Israel inajiandaa kwa
lolote lile.

Imeandaliwa na........

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment