Facebook

Saturday, 12 July 2014

Ukatili mwingine Morogoro



Wakati jamii ikiwa bado
haijasahau mateso aliyoyapata
mtoto Nasra Mvungi na
kusababisha kifo chake, tukio
lingine la aina hiyo limetokea
katika Kijiji cha Matongola, Tarafa
ya Magole Wilaya ya Kilosa, baada
ya kubainika mtoto wa miaka sita
akiwa amefichwa uvunguni mwa
kitanda na kufanyiwa vitendo vya
kikatili na mama yake mzazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Morogoro, Leonald Paulo alikiri
kutokea kwa tukio hilo na kusema
kuwa taarifa za mateso ya mtoto
huyo zilifikishwa Kituo cha Polisi
wilayani Kilosa za saa za mchana
jana, baada ya uongozi wa kijiji
na kata kutoa taarifa na tayari
mwanamke huyo amekamatwa
kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Mama aliyefanya ukatili huo
anafahamika kwa jina la Sala
Mazengo ambaye alimficha ndani
mtoto wake aliyefahamika kwa
jina la Devota Malole na
kumfanyia vitendo vya kikatili
ikiwa pamoja na kutompa chakula,
wala kumfanyia usafi.
Baada ya kufichuliwa kutoka
alipofichwa, mtoto huyo
alionekana kuwa dhaifu kiafya
kutokana na kukosa lishe pamoja
na mazingira aliyokuwa akiishi
kutoridhisha, jambo ambalo ni
kosa kisheria, pia ukiukwaji wa
haki za watoto.
Inadaiwa kuwa tangu mwka 2009
Sala amekuwa akimficha mtoto
wake huyo ambaye sasa amelazwa
katika Hospitali ya Wilaya ya
Kilosa kwa ajili ya kupatiwa
vipimo na matibabu.
Hata hivyo, mwanamke huyo
alipoulizwa alidai kuwa afya ya
mtoto wake ilikuwa mbaya tangu
alipozaliwa kutokana na
magonjwa ya mara kwa mara, pia
hali ngumu ya maisha ilichangia
kudhoofisha afya ya mtoto huyo.
Alidai kuwa ana watoto sita, pia
alikiri kumlaza chini mtoto huyo
kutokana na kuwa na kitanda
kimoja, ambacho hakiwatoshi
watoto hao.
Aliongeza kuwa hata chakula
amekuwa akikipata kwa shida
kutokana na kushindwa kufanya
kazi kwa kuwa ana mtoto
mwingine mdogo.
Kamanda Paulo alisema kuwa
mwili wa mtoto huyo umedhoofu
kutokana na kufichwa ndani kwa
muda mrefu na bado mwanamke
huyo hajaeleza sababu za kufanya
vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto
huyo.
“Siwezi kutoa taarifa ya kidaktari,
lakini kutokana na afya ya mtoto
yule na mazingira tuliyomkuta ni
dhahiri alikuwa akipata mateso na
kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Hata hivyo, uchunguzi zaidi
tunaufanya na kwamba taratibu
za kumfikisha mtuhumiwa huyo
Kituo Kikuu cha Polisi mkoani
hapa zinaendelea,” alisema
Kamanda Paulo.
Alisema kuwa mpaka sasa bado
haijafahamika kama mtoto Davota
ni mlemavu au la na kwamba
taarifa za afya ya mtoto huyo
zitatolewa baada ya madaktari
kumfanyia uchunguzi wa kina.


Kutoka kwa........Mdau BantuTz

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment