Facebook

Wednesday, 9 July 2014

Kilichojiri kuhusiana na kesi inayomkabili Oscar Pistorius

UTETEZI WAKAMILISHA HOJA KATIKA KESI YA PISTORIUS
Upande wa utetezi katika kesi ya mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius umemaliza kuwasilisha hoja zake za utetezi. Wakili wake, Barry Roux amesema amemaliza kuita mashahidi. Lakini amesema baadhi ya mashahidi hawakutaka kutoa ushahidi wao kutokana na umaarufu wa kesi hiyo na kufuatiliwa kwa karibu na vyombo vya habari. Pistorius anatuhumiwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi zilizopenya kwenye mlango wa msalani, nyumbani kwake. Amesema alidhani ni mwizi ameingia nyumbani kwake. Jaji ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe saba mwezi Agosti. 

Upande wa utetezi katika kesi ya mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius umemaliza kuwasilisha hoja zake za utetezi. Wakili wake, Barry Roux amesema amemaliza kuita mashahidi. 

Lakini amesema baadhi ya mashahidi hawakutaka kutoa ushahidi wao kutokana na umaarufu wa kesi hiyo na kufuatiliwa kwa karibu na vyombo vya habari. 

Pistorius anatuhumiwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi zilizopenya kwenye mlango wa msalani, nyumbani kwake. Amesema alidhani ni mwizi ameingia nyumbani kwake. Jaji ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe saba mwezi Agosti.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment