Luiz akilia baada ya kushindwa na Ujerumani
Nahodha wa muda wa Brazil David
Luiz amewataka mashabiki wa tim,u hiyo kote duniani kuwasamehe
wachezaji waliokuwa uwanjani Selecao ilipoadhibiwa kichapo cha mabao
7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la
dunia huko Brazil.
Amini Usiamini Ujerumani ilikuwa inaongoza mabao 5-0 kufikia dakika 29 ya kipindi cha kwanza .Luiz,ambaye alitajwa kama nahodha wa muda baada ya marufuku ya Nahodha Thiago Silva kumlazimu kutizama tu mechi hiyo alisema hawjui kilichotendeka lakini ni wakati wao kujifunza kutokana na aibu hiyo ya kusakamwa 7-1. "Ni siku ya majonzi tele kwa wabrazil''.
Luiz akilia baada ya kushindwa na Ujerumani
Kilio kimezidi kote nchini humo haswa baada ya nyota wa Brazil Neymar kujeruhiwa uti wa mgongo Ijumaa iliyopita katika mechi ya kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya Colombia.
Kwa Upande wake Kipa wa Brazil Julio Cesar alitaja dakika hizo kumi timu hiyo ilipofungwa mabao manne kuwa sawa na kuzimia.
''Sio jambo unaloweza kujieleza.
Julio Ceasar; Ujerumani ilikuwa timu bora
Hata hivyo tunawashukuru Wabrazil kwa kutuunga mkono katika kipindi hichi chote .
Hata wachezaji wakiomba msamaha kwa kichapo hichi cha leo ,ni wazi kuwa mjerumani alituzidi maarifa .
Lazima tukubali hilo walikuwa bora kuliko sisi leo.'''
0 comments:
Post a Comment