
Liverpool inafikiria kumsajili mshambuliaji wa AC Milan Mario Balotelli, iwapo Luis Suarez atajiunga na Barcelona (Daily Express),
Wakati huohuo Brendan Rodgers anamtaka beki Dejan Lovren kuwa mchezaji
wa tatu kutoka Southampton kwenda
Anfield, baada ya kumchukua Lambert na Lallana (Times),
Kiungo wa
Colombia James Rodrigues anajiandaa kuondoka Monaco kwenda Real Madrid
kwa pauni milioni 40, iwapo Real watamuuza Angel Di Maria (Daily Mail),
Arsenal watathibitisha kumsajili Mathew Debuchy kutoka Newcastle baada
ya Kombe la Dunia (Daily Star),
Mshambuliaji wa Porto Jackson Martinez
amekiri kuwa angependa kujiunga na Arsenal, klabu ambayo alikuwa
akiishabikia akiwa mtoto (Daily Express),
Manchester City wamekubaliana
na Roma kumsajili beki wa kati Mehdi Benatia, lakini watasubiri Roma
wapate mtu wa kuziba pengo (Daily Mirror),
kipa wa Costa Rica, Keylor
Navas anajiandaa kuhamia England baada ya Arsenal nao kujiunga na
Liverpool kumsaka (Daily Star),
Manchester United watatoa pauni milioni
20 kumsaka beki wa Borussia Dortmund Mats Hummels wiki hii (Metro).
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Endelea kutembelea www.bantutz.com kupata taarifa zinazohusiana na usajili barani Ulaya kwa muda na wakati muafaka.
0 comments:
Post a Comment