Facebook

Thursday, 3 July 2014

Tohara yasababisha vifo vya vijana 19 Afrika Kusini


Wizara ya Afya nchini Afrika Kusini inasema kuwa wavulana kumi na tisa wameaga dunia mwaka huu katika sherehe za kitamaduni za kuwapasha tohara wavulana.
Tohara hiyo ni utamaduni unaopewa heshima kubwa katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo.
Utamaduni wa tohara ni muhimu kwa vijana hasa kwa kuwa ni njia ya vijana kuingia utu uzima, lakini baadhi hufariki wakipitia utamaduni huo na wengine hupoteza sehemu zao nyeti.
Vijana 19 wamefariki kufika sasa na wengine 50 wako hospitalini.
Wanapokea matibabu ya kukosa maji mwilini, sehemu zao za siri kuoza na majerahe mengine mabaya.
Wazee wa kijamii wasiokuwa na mafunzo ya kufanya tohara ambao huendesha vituo vya kuwapasha tohara vijana wamelaumiwa kwa vifo kama hivyo.
Katika baadhi ya visa ambavyo vimeripotiwa, vijana hutoroka na kujiunga na vijana wengine wanaokwenda katika vituo hivyo haramu bila ya idhini ya wazazi.
Serikali imewasihi wazee wa kijamii kushirikiana na watu wenye uwezo wa kitaalamu na madaktari ili kuwapasha tohara vijana na kuzuia vifo.
Mwezi jana watu 23 walikamatwa kwa vifo vya vijana waliofariki kutokana na athari za kupashwa tohara.

Related Posts:

  • Mlipuko waua watu 10 nchini Nigeria Takriban watu 10 wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika mji wa Bauchi Kaskazini mwa Nigeria. Kwa mujibu wa polisi, shambulizi hi… Read More
  • Wagonjwa wa Ebola watoroka hospitalini Watu zaidi ya miatano tayari wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika kanda ya Afrika Magharibi Serikali ya Sierra Leone imeonya kuwa ni … Read More
  • Uingereza yaomba ruhusa ya jeshi lake Wanajeshi wa Uingereza Uingereza imesema kuwa inafanya mazungumzo na kenya ili kutatua mzozo kuhusu mafunzo ya wanajeshi wa Uingereza nchini humo. Serikali ya Kenya inaaminika kuchelewa kuwaruhusu wanajeshi zaidi wa … Read More
  • Alazwa hospitalini baada ya kumkana Mungu Mubarak Bala Mwanamume mmoja katika jimbo la Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha matibabu ya kiakili baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika moj… Read More
  • Wanajeshi wa Iraq wauteka mji wa Tiqrit Wanajeshi wa Iraq wakielekea mjini Tiqrit Serikali ya Iraq inasema kuwa vikosi vyake vimeuteka mji wa kazkazini wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji wa ki-sunni ambao walikuwa wameteka mji huo wiki mbili zilizopita. Vyo… Read More

0 comments:

Post a Comment