Mashambulio ya anga kwenda Gaza na maroketi kwenda Israel yameendelea
wakati harakati za Israel dhidi ya wapiganaji wa Palestina zikiingia
siku ya saba.
Maafisa wa Palestina wanasema watu 172 wameuawa Gaza tangu mapigano hayo yaanze Jumanne iliyopita.
Israel inasema karibu maroketi 1,000 wamevurumishwa kutoka Gaza katika kipindi hicho. Imesema imedondosha chombo kimoja cha anga cha Palestina karibu na Ashdod siku ya Jumatatu asubuhi.
Maelfu ya watu wamekimbia makazi yao kaskazini mwa Gaza baada ya onyo kutolewa na Israel.

Israel imeweka maelfu ya wanajeshi wake katika mpaka na Gaza na kutoa onyo huku ikijiandaa mashambulizi ya ardhini.
Makomando wa Israel wameendesha shambulio la kwanza la ardhini siku ya Jumapili, na kushambulia kituo kinachodhaniwa ni cha kurushia maroketi.
0 comments:
Post a Comment