Kampuni ya Adidas imesaini mkataba wa pauni milioni 750 wa kutengeneza
jezi za Manchester United kwa miaka kumi kuanzia msimu ujao.
Hatua hii imekuja baada ya mahasimu wao wa Marekani, Nike, kuamua kutoendelea na klabu hiyo mwishoni mwa msimu wa 2014-15.
Hatua hii imekuja baada ya mahasimu wao wa Marekani, Nike, kuamua kutoendelea na klabu hiyo mwishoni mwa msimu wa 2014-15.
Nike imekuwa ikiilipa United pauni milioni 23.5 kwa mwaka lakini mkataba huu mpya umevunja rekodi, kwa kulipa pauni milioni 75 kwa msimu, Old Trafford.
Mkataba wa Adidas na mabingwa wa Champions League, Real Madrid wa pauni milioni 31 kwa mwaka ndio ulikuwa mkubwa zaidi.

Awali Nike ilipewa muda wa miezi sita kufikiria iwapo inataka kuendelea kuwa na United.
0 comments:
Post a Comment