Facebook

Thursday, 3 July 2014

Origi mbioni kutua Uingereza.


Mchezaji wa zamani wa klabu ya Gor Mahia na timu ya taifa ya Kenya Haraambee Stars, Austin Oduor, amesema mshambuliaji matata wa timu ya taifa ya Ubelgiji Divorc Origi ameiva kucheza katika ligi kuu ya England.
Oduor, ambaye ni mjomba wake Origi, anasema tofauti na maoni ya wengine kwamba mchezaji huyo angali mbichi kucheza ligi kuu ya England kwake yeye anaona yuko tayari kabisa.
“Nimefuatilia mechi zote alizocheza kufika sasa katika kombe la dunia na sina shaka kijana huyu wa ndugu yangu(Mike Okoth) anaweza kucheza ligi kuu ya England bila tatizo kwa sababu ana mwili mzuri, nguvu, akili ya mshambuliaji na kasi itakikanayo kwa ligi kama hiyo,’’ asema Oduor.
''Asipoteze muda wake kwa sababu huu ndio umri mzuri kwake kushiriki ligi hiyo. Nitazungumza naye na babake baada ya kombe la dunia kwani singetaka tuanze kuzungumzia mengine wakati huu ila kombe la dunia tu.’’
Baadhi wanahisi kuwa Origi bado ni mbichi ingawa ameonyesha kipawa chake Brazil
Origi, mwenye umri wa miaka 19 ameonyesha mchezo mzuri kwenye mashindano ya kandanda ya kombe la dunia nchini Brazil, na kwa mara ya kwanza alicheza dakika zote tisini dhidi ya Marekani kwenye mechi yao ya raundi ya pili, na hatimaye Romelu Lukaku akaingia uwanjani naye Origi akapumzika.
Miongoni mwa timu za ligi kuu ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili Origi ni Liverpool, Tottenham Hotspurs na Arsenal lakini kuna dalili Liverpool itamnasa kinda huyo ambaye alizaliwa Ubelgiji wakati babake Mike Okoth, raia wa Kenya, alipokuwa akicheza kandanda ya kulipwa nchini humo.
Origi mwenyewe anasema ana hamu sana ya kushiriki ligi kuu ya England bora apate klabu kitakachomfurahisha.
Babake Origi ni shabiki sugu wa Liverpool hivyo basi huenda akamshawishi mwanawe ajiunge na bingwa hao mara 18 wa ligi kuu ya England.
Lakini kabla mashindano ya kombe la dunia yaanze Okoth alisema atampa Origi uhuru wa kuamua ni klabu kipi anataka kuchezea England endapo atakiacha kile cha Ufaransa, Lille.

Related Posts:

  • Man City yamnyatia Isco.Manchester City inataka kupata saini ya kiungo wa Real Madrid Isco. Mchezaji huyo miaka 23 hajui hatima yake Santiago Bernabeu baada ya ujio wa meneja mpya Rafa Benitez.Isco alijiunga na Real Madrid kwa ada ya Euro milioni30 … Read More
  • Yaya Toure 'Siondoki Man City'Mchezaji Yaya Toure amethibitisha kuendelea kukipiga Manchester City msimu ujao, na anafuraha na heshima kwake kuendelea kuwepo Etihad pamoja na kuwepo na uvumi wa kuhamia timu ya Inter Milan ya Italy.Kiungo huyo miaka 32 … Read More
  • Schneiderlin kutua Man United kwa ada ya Euro milioni 25Manchester United imevutiwa na kutaka kumsaini mchezaji kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin..Kiungo huyo wa miaka 25 ni mmoja wa viungo waliocheza vizuri msimu uliomalizika wa Premier League.Timu ya Arsenal na Tottenha… Read More
  • Chelsea yarusha ndoano kwa Gundogan.Timu ya chelsea inatajwa katika mbio za kuhitaji saini ya mchezaji IIkay Gundogan kutoka Dortmund lakini taarifa zinasema mchezaji huyo yupo katika mazungumzo na vilabu vingine vya Barcelona, Manchester United.Bayern na Ars… Read More
  • Van Persie hatihati kusalia Man United Mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie amekubali kuondolewa Old Trafford baada ya kupitia magumu msimu huu.Mshambuliaji wa Manchester United ana mwaka mmoja tu wa kumaliza mkataba wake wa sasa.Van Persie ana ma… Read More

0 comments:

Post a Comment