Barcelona wataanza mazungumzo na Liverpool siku ya Jumatano (Leo) kuhusiana na uhamisho wa Luis Suarez.
Maafisa kutoka klabu hizo mbili watakutana London kujadili mkataba wa mshambuliaji huyo raia wa Uruguay. Suarez, ambaye amesalia na miaka minne kwenye mkataba wake na Liverpool, anatumikia adhabu ya miezi minne kwa kumng'ata Georgio Chiellini wa Italy wakati wa Kombe la Dunia.

Liverpool
huenda wakakubali kitita cha pauni milioni 80 kwa ajili ya Suares,
ambaye alijiunga na Liverpool kutoka Ajax kwa pauni milioni 22.7 mwaka
2011. Hata hivyo inaaminika kuwa Barcelona wanataka kutoa karibu pauni
milioni 60. Mkataba wowote huenda ukategemea iwapo Barcelona itamtoa
Alexis Sanchez kama sehemu ya kumchukua Suarez.
Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata taarifa zote zitakazokuwa zinahusiana na usajili katika kipindi hiki cha uasajili barani Ulaya.
0 comments:
Post a Comment