
Kiungo mshambuliaji wa Brazil na Chelsea, amesema hajui nini kimewatokea baada ya mfululizo wa matokeo mabaya katika mashindano ya Kombe la Dunia huko nchini kwao.
Hata hivyo, alikubali timu yao haikucheza vyema na itabidi kuangalia kwa undani zaidi mbinu zao ili kujirekebisha kwa baadae. Alisema
“Itabidi tufanye uchunguzi zaidi kujua nini hakikuwa sawa kwenye timu yetu, ili tuweze kujirekebisha kwa baadae. Kwa kweli najisikia vibaya sana, sijui nini cha kusema"
"Baada ya kupoteza dhidi ya Wajerumani, jana nadhani tulijitahidi kucheza vyema kutoka mwanzo wa mchezo ili kunyakua nafasi ya mshindi wa tatu, lakini nadhani haikuwa siku yetu" Alimalizia Oscar
0 comments:
Post a Comment