Liverpool wamekubali yaishe katika jaribio lao la kumsajili straika wa Barcelona , Alexis Sanchez,25.
Viongozi wa The Reds walifanya mazungumzo na mchezaji huyo raia wa Chile, wakitaraji wanaweza kumshawishi kuhamia Anfild lakini wakaondoka patupu kwa kuambiwa straika huyu kuna kila dalili ya kwamba atajiunga Arsenal kwa kua ndio chaguo lake Premier League.
Hilo limefuatia kujulishwa kwamba Sanchez angependa kukipiga Premier League na hivyo Liverpool kudhani wana nafasi ya kumshawishi kwa kua nao pia wapo Premier League. Lakini jibu lilikua kwamba si tu Premier League bali pia angependa kuichezea Arsenal.
Kwa sasa Liverpool wajiandae kukutana nae dimbani dhidi yao katika Premier League msimu unaofuata, kwa sasa taarifa zinasema kwamba straika huyo yupo karibu kabisa kukamilisha taratibu za kujiunga na Arsenal kwa dau linalosemekana kua £30million na itatangazwa rasmi hivi karibuni.
Page hii ya Arsenal Tanzania hua haiandiki habari zisizo na uhakika na kama habari ikiwa tofauti basi hua tunawapa sababu.
Baadhi ya mashabiki wanaamini kua Sanchez ameshahamia Arsenal, ukweli ni kwamba suala hilo bado kukamilika ingawa pande zote tatu zimeshafikia makubaliano. Tukumbuke sakata la Higuain, na hata hivi karibuni Willian tulimuona hadi akifanya vipimo vya afya katika klabu ya Tottenham ila baadae akatangazwa ni mchezaji wa Chelsea. Cha msingi mchezaji si mchezaji wa timu yoyote mpaka timu hiyo ipate saini yake na kwa sasa Sanchez bado kutia saini ingawa makubaliano yote yameshafikiwa.
Kwa hiyo fuatilia hapa ama vyanzo rasmi vya kuaminika vya Arsenal.

0 comments:
Post a Comment