Rais wa Brazil Dilma Rousselff ameitaka nchi yake 'kujinyanyua' baada
ya kichapo cha mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani katika Kombe la Dunia.

"Kama Wabrazil wote, nimesikitishwa sana sana baada ya kufungwa. Lakini hatutosononeka," rais huyo ame - tweet.
Kocha wa Brazil Luiz Filipe Scolari amesema kupoteza mchezo huo ilikuwa "siku yake mbaya zaidi maishani mwake".
Vyombo vya habari vya Brazil vimeandika habari za jinsi watu
walivyopokea mshtuko huo wa matokeo siku ya Jumatano, vikieleza matokeo
hayo kuwa ni "udhalilishwaji wa kihistoria". Matokeo hayo ni mabaya zaidi katika historia ya Brazil katika Kombe la Dunia.Endelea kutembelea www.bantutz.com kupata habari mbalimbali kwa muda na wakati muafaka.

0 comments:
Post a Comment