Alvaro Negredo anataka kuondoka Manchester City na huenda akarejea
Spain. City wamesisitiza kuwa mshambuliaji huyo hauzwi, lakini inafahamika
kuwa anataka kujiunga na Atletico Madrid (Daily Mail),
Manchester
United wameambiwa wanaweza kumsajili kiungo William Carvalho kutoka
Sporting Lisbon, lakini lazima walipe pauni milioni 37 kutegua kizingiti
cha ununuzi (Daily Express),
Everton wamekataa ombi la Tottenham
kumsajili beki John Stones (Sun),
Southampton wamedhamiria kumshikilia
beki wao wa kati Dejan Lovren anayenyatiwa na Liverpool, Tottenham na
Arsenal (Daily Express),
Juventus wanataka kumchukua beki wa kati wa Man
City Matija Nastasic kwa mkopo ili kuziba pengo la Andrea Barzagli
ambaye amefanyiwa upasuaji (talksport),
Mshambuliaji wa zamani wa
Chelsea Samuel Eto'o huenda akasalia EPL- Arsenal na Everton wanafikiria
kumchukua (Talksport),
Beki wa Atletico Madrid Filipe Luis atalazimika
kulazimisha uhamisho wake kwenda Chelsea baada ya mazungumzo kati ya
timu hizo mbili kudorora (Daily Star),
Arsenal na Liverpool watagombea
kusaka saini ya nyota wa Chile na Barcelona Alexis Sanchez ambaye huenda
akagharimu pauni milioni 30 (Daily Mail),
Harry Redknapp amekuwa
akizozana na wakuu wa QPR kuhusiana na kutaka kumsajili Rio Ferdinand
aliyekuwa Man United (Daily Mirror),
Galatasaray wametoa mkataba wa
pauni milioni 3 kwa msimu kumshawishi Samuel Eto'o (Le Figaro),
Diego
Maradona atafanya mazungumzo kuhusiana na kupewa kazi ya kuifundisha
timu ya taifa ya Venezuela (Guardian),
Hatimaye mshambuliaji wa
Tottenham Emmanuel Adebayor tayari ameanza mazoezi kujiandaa na msimu
mpya- na zoezi zaidi analofanya ni mitindo mipya ya kushangilia goli.
Tafadhali share tetesi hizi- Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata tetesi zote zinazohusiana na usajili barani Ulaya kwa muda na wakati mufaka.
0 comments:
Post a Comment