Kundi la al-Shabab limesema limempiga risasi na kumuua mbunge mmoja maarufu mjini Mogadishu.
Ahmed Mohamud Hayd aliuawa na watu waliokuwa ndani ya gari, wakati akitoka katika hoteli aliyofikia katika eneo linalolindwa vikali, wamesema watu walioshuhudia.
Mlinzi wake pia ameuawa na msaidi mmoja kujeruhiwa.
Mwandishi mmoja mjini Mogadishu Mohammed Moalimu amesema mauaji ya Bwana Hayd- ambaye ni kamanda wa zamani wa kijeshi na pia waziri - yameshtusha watu wengi.
0 comments:
Post a Comment