Arsenal watakamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Chile, Alexis
Sanchez, 25 anayechezea Barcelona siku ya Jumatano, kwa mujibu wa Arsene
Wenger (Talksport),
Tottenham wametoa dau jipya na 'kuuteka' mchakato
wa Liverpool wa kumsajili kiungo wa
Lille Divock Origi (Daily Mirror),
Juventus wamewasilisha tena dau la
pauni milioni 2 kumsajili beki wa Manchester United Patrice Evra, 33
(daily Mail),
Iwapo Evra atakwenda Turin, kiungo kutoka Chile, Arturo
Vidal, 27, huenda akaweza kwenda Old Trafford kwa kitita cha pauni
milioni 32 (Daily Express),
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Eduardo,
31, amewaaga wachezaji wenzake wa Shaktar Donetsk huku kukiwa na taarifa
kuwa atajiunga na Flamengo ya Brazil (Sky Sports),
Roma na Napoli za
Italia pamoja na mabingwa wa Ubelgiji Anderlecht wamepanda dau kumsajili
beki wa kulia wa Marekani DeAndre Yedlin, 21, ambaye aliichezea Seattle
Sounders ya Marekani msimu uliopita (Sky Sports),
Paris St-Germain wapo
tayari kutoa pauni milioni 70 kumnunua kiungo mfaransa Paul Pogba, 21,
kutoka Juventus (Le Figaro),
Juventus pia wanakaribia kumsajili
mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 21 (Marca)
Mshambuliaji wa
zamani wa Chelsea Didier Drogba, 36, anasuburi huenda Juventus wakamuita
baada ya kumaliza mkataba wake na Galatasaray ya Uturuki (Tuttosport),
Arsenal wanakaribia kupata saini ya Loic Remy kutoka QPR. Timu hizo
mbili karibu zinakamilisha makubaliano juu ya ada ya uhamisho, ingawa
Remy bado hajazungumzia maslahi binafsi na Gunners (Daily Mirror),
Baada
ya kukamilisha mikataba ya Alexis Sanchez na Mathiew Debuchy, mchezaji
mwingine anayesakwa na Arsenal ni kiungo wa Real Madrid Sami Khedira.
Los Bloncos watamruhusu Khedira kuondoka baada ya kufanikisha uhamisho
wa Toni Kroos (Daily Express),
Manchester United wanajiandaa kumnyatia
Ricardo Rodriguez anayechezea Wolfsburg, kuziba nafasi ya Patrice Evra
(Magazeti mbalimbali),
Atletico Madrid wamekubaliana na Bayern Munich
juu ya Mario Mandzukic kwa kitita cha euro milioni 22 (Bild),
Everton
wanataka kumsajili kwa mkopo Demba Ba kutoka Chelsea (Daily Star),
Nicklas Bendtner anatarajiwa kusaini katika timu mpya wiki hii baada ya
kuruhusiwa kuondoka na Arsenal (BBC)
Winga wa Manchester United,
Adnad Januzaj, 19, amepata vitisho kufuatia uamuzi wake wa kuichezea
Ubelgiji badala ya Albania au Kosovo, kwa mujibu wa taarifa kutoka
Serbia (Daily Mail).
0 comments:
Post a Comment