
Maafisa wakuu wa usalama na wa polisi wamefukuzwa kazi kufuatia kundi la al-Shabab kushambulia ikulu ya Somalia, amesema waziri mmoja.
Washambuliaji watatu waliuawa na wa nne kukamatwa, imesema ofisi ya rais.
Al-Shabab waliingia katika eneo la ikulu ya rais siku ya Jumanne kabla ya kukabiliana na kufukuzwa na majeshi ya Umoja wa Afrika na majeshi ya serikali.
Hili lilikuwa shambulio la pili zito mwaka huu katika eneo hilo linalolindwa vikali.
Mkuu wa polisi na mkuu wa Usalama wa taifa - Abdihakim Saaid na Bashir Gobe, wamefukuzwa kazi na nafasi zao kuchukuliwa na maafisa wengine, amesema waziri wa habari, Mustafa Dhuhulow.
Rais Hassan Sheikh Mohamud hakuwepo ndani ya Ikulu wakati wa shambulio hilo.
Al-Shabab wamesema wanajeshi 14 waliuawa katika mapigano hayo, lakini maafisa wa serikali hawakutaka kuzungumzia madai hayo.
0 comments:
Post a Comment