TETESI ZA SOKA ULAYA

Mshambuliaji wa Uholanzi na Bayern Munich Arjen Robben, 30, amekataa 'ofa' ya kujiunga na meneja wake Louis van Gaal, Old Trafford (Daily Telegraph),

Mshambuliaji wa Uholanzi na Bayern Munich Arjen Robben, 30, amekataa 'ofa' ya kujiunga na meneja wake Louis van Gaal, Old Trafford (Daily Telegraph),
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ana matumaini ya
kukamilisha usajili wa kipa wa Colombia
David Ospina, 25, kutoka klabu ya Nice wiki hii (Daily Mirror),
Chelsea
wameanza mazungumzo kuhusu kumrejesha Didier Drogba, 'Darajani' kuwa
mshambuliaji wa akiba na kocha (Daily Mail),
Mshambuliaji wa Liverpool
Iago Aspas, 26, anajiandaa kujiunga na Sevilla kwa mkopo msimu wote ujao
(Liverpool Echo),
Mipango ya uhamisho ya Tottenham imekwama kwa sababu
kiungo Gylfi Sigurdsson, 24 na beki Michael Dawson, 30, hawataki
kuondoka (Daily Mirror),
Wakala wa beki wa Spurs Jan Vertonghen, 27,
amekiri kuwa mchezaji huyo huenda akaondoka White Hart Lane (Evening
Standard),
Liverpool wameanza tena kumfuatilia beki wa kushoto wa
Sevilla Alberto Moreno (Daily Express),
kocha wa Marekani Jurgen
Klinsmann amesema amekataa 'ofa' kibao kutoka Ulaya, ikiwemo Galatasaray
(Le Figaro),
Mshambuliaji wa Monaco, James (inatamkwa Hamez) Rodrigues,
23, amesisitiza kuwa anataka kuichezea Real Madrid, akisema ni juu ya
rais wa klabu hiyo kufanya uamuzi (Marca),
Lazar Markovic atafanya
vipimo vya afya Liverpool Jumatatu, kabla ya kukamilisha uhamisho wake
wa euro milioni 25. Brendan Rodgers anataka kumchukua pia Wilfried Bony
kuziba nafasi ya Luis Suarez (Daily Telegraph),
Boss wa Chelsea Jose
Mourinho anataka kumchukua Sami Khedira. Arsenal walikuwa wakimtaka
mchezaji huyo, lakini sasa wataanza kumfuatilia zaidi Lars Bender (Daily
Mail),
Liverpool huenda ikaingia Southampton tena, safari hii wakimtaka
Jay Rodriguez kuchukua nafasi ya Iago Aspas (Daily Mail),
Manchester
United inakaribia kumsajili kiungo kutoka Chile, Arturo Vidal
anayechezea Juventus. United wamekubaliana ada ya uhamisho ya euro
milioni 40, na kuhama kwa Patrice Evra kwenda Juve (Marca),
Juventus
watamfuatilia Paulinho kutoka Tottenham iwapo watamuuza Arturo Vidal
(Daily Express),
Manchester United watakabiliwa na ushindani kutoka
Barcelona kumsajili beki wa kati wa Borussia Dortmund Mats Hummels. Luis
Enrique anamtaka Hummels baada ya mazungumzo ya kumsajili Marquinhos
kuvunjika (Daily Star).
0 comments:
Post a Comment