Facebook

Monday, 14 July 2014

UFARANSA KUUNDA JESHI KUPAMBANA NA MAKUNDI YA JIHAD

Ufaransa itaanzisha shughuli mpya za kijeshi katika eneo la Sahel, Afrika Kaskazini, katika juhudi za kuzuia kuibuka kwa makundi ya jihadi.
Takriban wanajeshi 3,000 watapelekwa huko, kwa pamoja na wanajeshi kutoka Mali, Mauritania, Burkina Fasi na Chad.
Siku ya Jumatatu, Ufaransa ilimaliza shughuli zake za kijeshi nchini Mali, zilizoanza miezi 18 iliyopita baada ya harakati za jihad kuibuka.
Majeshi ya Ufaransa yalisaidia serikali ya Mali kudhibiti upande wa kaskazini mwa nchi uliochukuliwa na wapiganaji wenye uhusiano na al-Qaeda mwaka jana.
Jeshi hilo jipya la muda mrefu, lijulikanalo kama 'Operation Barkhane' litaweka kambi yake katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena, lakini litakuwa na uwezo wa kufanya shughuli zake nje ya mipaka.
Majeshi ya Ufaransa yatakuwa na ndege sita za kijeshi, helikopta 20 na ndege tatu zizizohitaji rubani.

0 comments:

Post a Comment