Facebook

Thursday, 17 July 2014

Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya.

Salim Kikeke's photo.
Chelsea wako tayari kumuuza John Obi Mikel kwa pauni milioni 5 na klabu kadhaa za Serie A za Italia zimeambiwa zinaweza kumchukua (Daily Mail),
 
Meneja wa Manchester City, Manuel Pellegrini amekataa kuzungumza na Chama cha Soka cha Brazil kuhusu kuchukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari kuifundisha timu ya taifa (El Mercurio),
 Salim Kikeke's photo.
 Real Madrid wamekubaliana na James Rodriguez. Real Madrid wana subiri kukubaliana na Monaco wanaotaka ada ya uhamisho kuwa euro milioni 80 (AS) 
 
West Ham watakamilisha usajili wa Enner Valencia siku ya Jumatano kwa mkataba wa euro milioni 15 (Daily Mail), 
 
Swansea wamekataa pauni milioni 8 zilizotolewa na Liverpool kumsajili Ben Davis (Daily Telegraph), 
 Salim Kikeke's photo.
Manchester United, Chelsea na Arsenal watatakiwa kutoa zaidi ya euro milioni 75 ili kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain, Edison Cavani (talkSPORT),
 
 Everton wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Fevencvaros, Muhamed Besic kwa pauni milioni 4 (Daily Mail),
 
 Trabzonspor ya Uturuki wanamfuatilia beki wa Liverpool Kolo Toute (Daily Mail), 
 
Newcastle wanakaribia kukamilisha usajili wa Emmanuel Rivière kutoka Monaco (Daily Mail), 
 
Hatua ya Manchester United kumtaka Arturo Vidal kwa pauni milioni 35 kumesababisha boss wa Juventus kujiuzulu kwa hasira (The Sun),
 
 Besitkas wanamtaka Demba Ba, 29, kwa mkopo huku wakitaka kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu baada ya msimu (Daily Mirror),
 
 AC Milan wanamtaka winga wa Manchester United Nani (Football Italia),
 
 Manchester United wanawafuatilia kwa makini kuwapa majaribio Joao Virginia, 15, aliyepewa jina la 'Cristiano Ronaldo mpya' na kipa Joao Virginia, 15, kutoka Porto (Skysports) 
 
Share tetesi hizi na wapenda soka. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Related Posts:

  • Mbeya City yazidi kubomolewa   Mara baada ya Peter Mwalyanzi pamoja na Deus Kaseke kuondoka katika timu hiyo baada ya kusajiliwa na vilabu vya Simba na Yanga leo tena wameondoka wengine. Pichani hapo ni Paul Nongwa na Anthony Matogolo leo wamej… Read More
  • Arsenal yamtengea dau Kondogbia.Hakuna timu ambayo ipo nyuma kupata wachezaji wazuri kwa ajili ya msimu ujao. Ukikaa nyuma muda wa usajili maisha hayatakua mazuri muda wa msimu ujao. Arsenal inakomaa kumpata mchezaji Kondogbia ambae pia anatakiwa na Inter m… Read More
  • Gundogan atua Man UnitedManchester united imezipiku timu za Bayern Munich na Barcelona kwenye vita ya kupata saini ya mchezaji wa Borussia Dortmund. Mchezaji huyo ambae anacheza sehemu ya kiungo amekubaliana mambo ya msingi na Manchester united. Gun… Read More
  • BantuTz MAGAZETINI:Soma kilichoandikwa katika kurasa zote za magazeti yote ya leo. MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusomana kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuhimu… Read More
  • Falcao akubali kutua Chelsea.Kama BantuTz tulivyo ripoti hapo mwanzoni kwamba mama yake Falcao alisema kwamba mwanae hana furaha ndani ya Manchester united. Kwa hiyo lazima alikua anatarajiwa kuondoka Old Trafford baada ya msimu kuisha. Habari ikufikie k… Read More

0 comments:

Post a Comment