
Liverpool watafanya jitihada za mwisho kujaribu kumshawishi Ashley Cole kujiunga nao (Mail on Sunday),
Taarifa nyingine zinasema Cole tayari
ameingia mkataba wa miaka mitatu na Roma ya Italy (Sunday People),


Everton
watatupilia mbali maombi ya Manchester City ya kumtaka Ross Barkley
(Liverpool Echo),
Boss wa Liverpool Brendan Rodgers atamruhusu Martin
Skirtel kuondoka iwapo atapata mtu wa kuziba nafasi yake, huku Dejan
Lovren wa Southampton akitazamwa kuchukua nafasi hiyo (Sunday Express),
Beki wa Newcastle Matheiu Debuchy amethibitisha kuwa atajiunga na
Arsenal msimu ujao (Sunday Express),
Newcastle wanatazama uwezekano wa
kumchukua beki wa kulia wa Ajax Ricardo van Rhijn kuziba nafasi ya
Debuchy (Metro),
Liverpool watapewa pauni milioni 75.5 na Barcelona za
kumnunua Luis Suarez (Sunday Mirror),
kiungo wa zamani wa Chelsea
FrankLampard anakaribia ktangaza kujiunga na New York City FC (Daily
Star Sunday),
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kumnunua, ama
kiungo wa Real Madrid Sami Khedira au Morgan Schneiderlin wa Southampton
(Sunday Mirror),
Juventus wanataka kulipwa pauni milioni 45 pamoja na
Luis Nani ikiwa Manchester United wanamtaka kiungo Arturo Vidal (Daily
Star Sunday),
Barcelona wamekataa kumsaini beki wa kati wa Liverpool,
Daniel Agger, badala yake Barca wanamtaka Mats Hummels (Mundo
Deportivo),
Juventus wanahaha kumsajili Alexis Sanches lakini
watalazimika kuuza wachezaji ili kupata fedha. Juve watakuwa tayaru
kuwauza Paul Pogba na Arturo Vidal (Tuttosport),
Liverpool huenda
wakatumia sehemu ya pauni milioni 70 za Suarez, kumnunua mshambuliaji wa
AC Milan Mario Balotelli, ambaye anataka sasa kurejea EPL (Tuttosport),
Newcastle United wanataka kumsajili winga wa Manchester United Wilfried
Zaha kwa pauni milioni 7. Zaha alinunuliwa na Man U kwa pauni milioni
15 (Daily Mirror),
Manchester United wamekataa ombi la Southampton la
kumsajili Javier Hernandez Chicharito (Sunday People).
Share tetesi hizi
wa wapenda soka na wa. Tetesi nyingine.
0 comments:
Post a Comment