Arsenal
wamepata matumaini zaidi ya kumsajili Sami Khedira, 27, baada ya kiungo
huyo kukataa kusaini mkataba mpya na Real Madrid (Daily Star),
Arsenal
pia wapo katika mazungumzo ya kumsajili Loic Remy kwa pauni milioni 8
kutoka QPR iliyopanda daraja (Independent),
Hata hivyo mazungumzo kati
ya Arsenal na Remy yanadaiwa kuvunjika baada ya Remy kutokubali maslahi
binafsi, huku Newcastle na Tottenham wakitaka kumchukua (Daily Mail),
Chelsea wanataka pauni milioni 8 kwa ajili ya beki Ryan Bertrand, 24,
ambaye ananyatiwa na Liverpool na Tottenham (Daily Express),
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Marouanne Chamakh, 30, amekubali
mkataba wa miaka miwili kusalia Crystal Palace, huku akikubali
kupunguziwa mshahara kiwango kikubwa (Guardian),
Liverpool wameingia
kwenye mbio sawa na Tottenham za kumsajili Wilfried Bony, 25, ambaye
Swansea wanamuuza kwa pauni milioni 20 (Talksport),
Lazio wanaamini wana
kipaumbele zaidi kumsajili Stefan De Vrij, 22, kutoka Feyenoord, ambaye
anasakwa pia na Manchester United (Daily Express),
kiungo wa Spain
Mikel Arteta, 32, hana nia ya kuhama Arsenal kwa mujibu wa wakala wake
Inaki Ibanez (Times),
Arsenal wana matumaini ya kukamilisha usajili wa
Javi Manquillo kutoka Spain na Mathieu Debuchy, kuziba nafasi za Bacary
Sagna na Carl Jenkinson (Daily Mail),
Everton huenda wakamsajili Muhamed
Besic, 21, raia wa Bosnia Herzegovina kwa euro milioni tano (Daily
Mirror),
kiungo wa Juventus amezua gumzo zaidi la kuhamia Chelsea baada
ya kuonekana katika mitaa ya Stamford Bridge (Daily Mail),
Manchester
United huenda wakamfuatilia Ben Davies kuziba nafasi ya Patrice Evra
(Daily Mail),
Chelsea wamejiunga na Arsenal na Liverpool kumwania
mshambuliaji wa Real Sociedad Antoine Griezman, 23 aliyekataa mkataba
mpya (Daily Express),
Mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata,
anatazamiwa kwenda Juventus kwa pauni milioni 17.5. Real Madrid watakuwa
na uwezo wa kumnunua tena baada ya mwaka mmoja kwa pauni milioni 23.8
(Daily Mail).
Hizo ndio tetesi za leo, share na wapenda soka wote.
Nyingine kesho tukijaaliwa. Chee
0 comments:
Post a Comment