Facebook

Friday, 11 July 2014

Wanasayansi wagundua mapya kuhusu Malaria

Kulingana na uchunguzi wa vimelea vinavyosababisha Malaria huweza kuishi kwenye  uboho (bone marrow) na kuepuka kinga za mwili na hivyo basi kusababisha maradhi.
Uchunguzi huu umedhihirishwa na bwana Marti ambaye alizungumza na shirika la habari la Uingereza, BBC.
Swala la vimelea hivyo kujificha kwenye uboho si jambo geni, lakini kundi la wanasayansi wakiongozwa na Profesa Matthias Marti katika idara ya Afya ya umma kule Harvard, Boston, walifichua hasa ambako vimelea hivyo hujificha na kutoa maonyesho.
Uzinduzi huu una umuhimu mkubwa kwa misingi kuwa umeleta ujuzi unaohitajika sana na huweza kupelekea kuundwa kwa dawa na kinga mpya za kukabiliana na vimelea hivyo ili kuzuia maambukizi.
Kwa mujibu wa wanasayansi huko Harvard, uchunguzi huu uliochapishwa na jarida la kisayansi la Science Translational Medicine, umeongeza ujuzi wa kibaiologia utakaotumika kuchunguza ugonjwa wa Malaria hata zaidi.
Vimelea vinavyosababisha Malaria huambukizwa hasa kupitia mbu, na husababisha vifo zaidi ya nusu kila mwaka ulimwenguni.
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Shirika la afya duniani, zinapendekeza kuwa Malaria ilisababisha vifo 600,000 mwaka wa 2012, na takriban asilimia 90 ya vifo hivyo vilitokea Afrika.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment