Facebook

Saturday, 5 July 2014

"Wanawake" wa Boko Haram wakamatwa

Hafsat Usman Bako ni mmoja wa wale waliokamatwa
Jeshi nchini Nigeria linasema limewakamata wanawake watatu ambao walikua wanawaandikisha wafuasi wanawake kwa kundi la Boko Haram.
Inadaiwa wanawake hao waliwalenga wajane na wasichana wadogo wakiwaahidi kuwachumbia kwa wafuasi wa Boko Haram.
Mwaandishi mmoja akiwa Abuja anasema inaelekea Boko Haram inajaribu kuwashawishi wanawake washiriki vilivyo katika mapambano yao.
Mwezi uliopita mshambuliaji mwanamke wa kujitoa mhanga alifariki alipojaribu kuishambulia kambo ya kijeshi katika jimbo la Gombe - tukio la kwanza aina hiyo nchini Nigeria.
Bomu hilo lililipuka alipokua akipekuliwa katika kituo cha usalama . Mwanajeshi mmoja pia aliuwawa.
Wanawake pia ni miongoni mwa wale waliokamatwa na kuzuiliwa katika miji ya Maiduguri kaskazini mwa Nigeria, eneo ambalo Boko Haram wanaungwa mkono kiasi .
Jeshi la Nigeria limewakamata wanawake wafuasi wa Boko Haram
Jeshi la Nigeria limesema wanawake watatu iliowakamata walikuwa ni wa tawi la upelelezi la Boko Haram.
Ilisemekana mmoja wao alikua ni mjane wa mpiganaji wa Boko Haram.
Kundi hilo la wanaharakati wa Kiislamu bado linawashikilia zaidi ya wasichana wa shule 200 iliowakamata mnamo mwezi wa Aprili katika mji wa Chibok katika jimbo la Borno .
Boko Haram inadai wapiganaji wake na jamaa zao waachiliwe kwa kubadilishana na wasichana.Serikali imelikataa dai hilo. .

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment