Facebook

Tuesday, 8 July 2014

Webb huenda akachezesha fainali Brazil

Refa muingereza anayefahamika kwa ukakamavu wake Howard Webb ni miongoni mwa waamuzi 15 walioteuliwa kusalia Brazil kushiriki mechi zilizosalia za kombe la dunia.
Webb mwenye umri wa miaka 42 ni miongoni mwa wale watakaotathminiwa kwa uwezo wao wa kuamua mechi zenye umuhimu mkubwa ikiwemo fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Webb pamoja na wasaidizi wake Mike Mullarkey na Darren Cann wamekwisha amua mechi mbili za kombe la dunia huko Brazil.
Webb ni kati ya waamuzi 15 waliosalia Brazil
Mpiga kipenga huyo alikuwa muamuzi katika mechi kati ya Colombia na Ivory Coast na pia mechi baina ya wenyeji Brazil na Chile.
Webb alijiimarisha wasifu wake mwaka wa 2010 alipoamua mechi ya fainali ya kombe la dunia baina ya uhispania na Uholanzi nchini Afrika Kusini .
Webb ndiye aliyeamua fainali ya kombe la dunia la mwaka wa 2010
Webb hata hivyo alilaumiwa kwa kukosa kumwadhibu mchezaji Nigel de Jong.
Na baada ya kutizama kanda za video Webb alikiiri kuwa alistahili kumwonesha mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kadi nyekundu .
Refa mmoja pekee kutoka Brazili, Sandro Ricci ndiye aliyesalia kuamua mechi zilizosalia za nusu fainali fainali na mechi ya kuamua mshindi wa tatu.
Mbali na Brazili Argentina, Ujerumani na Uholanzi ndiyo mataifa yaliyosalia katika kipute hicho.
Refa Marco Rodriguez ndiye aliyakosa tukio la Suarez kumng'ata Chiellini
Refara kutoka Mexico Marco Rodriguez ndiye atakayeamua mechi ya kwanza ya nusu fainali kati ya Ujerumani na wenyeji Brazil.
Mechi hiyo itachezwa Jumanne .
Rodriguez ndiye refarii ambaye alikosa kumuona mshambulizi wa Uruguay Luiz Suarez akimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini.

Related Posts:

  • Habari za Michezo Kutoka Bongofun.blogspot.com ARSENAL WATAWALA KIKOSI CHA ENGLAND,MRUNDI BERAHINO NAYE NDANI Wayne Rooney na Wilshere                     &nbs… Read More
  • Liverpool vs Chelsea:LIVE COMMENTARYLIGI KUU ENLGAND: LEO KUANZIA SAA 9 DAK 45 MCHANA LIVERPOOL v CHELSEA VIKOSI: Liverpool: Mignolet; Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno: Can, Henderson, Gerrard; Coutinho, Sterling, Balotelli. Kiba: Brad Jones, Toure, Lambert, Lal… Read More
  • BantuTz LIVESTREAMING::->Liverpool Vs ChelseaAngalia live kupitia Computer au Tablet yako mechi kati ya Liverpool dhidi ya Chelsea Utaangalia mechi hiyo bila kukwama au kukatika kwa matangazo ya mechi hiyo hata kidogo. Utafurahia kuangalia mechi hiyo kama utatumia Compu… Read More
  • UCHAMBUZI:LIVERPOOL vs CHELSEATAREHE 8 NOVEMBA 2014 LIGI KUU YA UINGEREZA LIVERPOOL  V  CHELSEA ANFIELD Saa 9:45 alasiri: HABARI ZA KILA TIMU KWA UFUPI: Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard anatarajiwa kuanza kwenye mechi ya Leo baada ya kuanzia… Read More
  • Mrundi aitwa kikosi cha Uingereza   Mshambuliaji wa klabu ya West Brom ya Uingereza, Saido Berahino ametajwa katika kikosi cha England kwa mara ya kwanza na meneja Roy Hogson. Berahino, 21, huenda akacheza mechi dhidi ya Slovenia ya kufuzu Euro 201… Read More

0 comments:

Post a Comment