Maafisa wa polisi nchini Brazil
wamemkamata afisa mkuu mtendaji wa kampuni mshirika wa FIFA kwa tuhuma
za uuzaji tiketi za kombe la dunia kinyume na kanuni.
Ray Whelan ambaye ni meneja mkuu mtendaji wa
kampuni mshirika wa FIFA Match Hospitality alikamatwa katika hoteli moja
huko Rio de Janeiro , inayotumika pia na maafisa wa shirikisho la FIFA.Polisi walisema kuwa kikundi hicho kilikuwa sehemu ya genge kubwa la kimataifa ambalo lilikuwa likiuza tiketi ambazo zilikuwa zimetengewa makundi maaluma ikiwemo tiketi zilizokuwa zimetengewa wachezaji .
Afisa wa Match Hospitality akamatwa Brazil
Kufuatia kashfa hiyo uchunguzi unaendelea kubaini iwapo baadhi ya tiketi hizo zimeuziwa watalii ambao hawakujua walikuwa wanakiuka sheria za shirikisho la soka duniani FIFA.
Kompyuta na vifaa vyengine vya kielektroniki vilikamatwa na polisi kwa uchunguzi zaidi kutopka kwa mkahawa huo wa kifahari ulioko Copa Cabana Palace Hotel
Tiketi za kombe la dunia zilikuwa zinauzwa kinyume na kanuni
Afisa anayeongoza uchunguzi huo Fabio Barucke, amesema kuwa afisa huyo alikuwa na hati zinazomruhusu kuingia katika afisi zote za fifa kwa hivyo alikuwa na uwezo wa kuzipata tiketi hizo.
Uchunguzi unaendelea.
0 comments:
Post a Comment