Vijana hufunzwa soka wakiwa wadogo na kukuwa wakiingia katika vilabu mashuhuri duniani
Timu ya Ivory Coast ni moja kati
ya timu za Afrika zilioanza vizuri katika michuano ya kombe la dunia
inayoendelea nchini Brazil mwaka huu kwa kuonyesha uwezo wake dhidi ya
Japan baada ya kuichabanga mabao 2-1.
Katika taarifa yake baada ya kutembelea taasisi
ya michezo kwa vijana nchini humo mwandishi mashuhuri Tamasin anagundua
siri ya kwanini wachezaji wa Ivory Coast wanacheza kwa viwango vya
kuridhisha katika michuano hii.Wachezaji wengi wa kimataifa kutoka nchini humo, walipitia katika kituo hiki na Issa amejiunga akiwa na miaka 15.
Ni moja ya vituo vyenye mafanikio makubwa kati ya shule za michezo. Yeye anazungumza na mwandishi Tamasin anayefuatilia siri ya mafanikio katika soka na maandalizi ya wachezaji tangia wakiwa wadogo.
'Soka kimataifa'
Ivory Coast inachanganya masomo na michezo ili kukuza vipaji vya vijana
Miaka mitatu iliyopita Julien Chevalier alijiunga katika kituo cha cha michezo cha ASEC Mimosifcom kama kocha anasema kituo hiki kimekuwa na ufanisi mkubwa na kutoa wachezaji wakubwa kwani tangia kuanzishwa kwake 1994 Asec imetoa wachezaji wanao ng’ara kimataifa na kidunia.
Hata hivyo baadhi ya wahitimu wa miaka ya hivi karibuni tayari wanawika katika soka la ulaya ambao ni kama Anderlecht's Gohi, Bi Cyriac ,Saint-Etinne's na Ismael Diomande.
'Ukuzaji wa vipaji'
''Kila mwaka kituo hiki kimekuwa kikisajili watoto wapatao 7000 toka maeneo mbalimbali nchini humu hapo tunatarajia kutengeneza akina Drogba wa siku zijazo’’,anasema Chevalier huku akitabasamu.
Zaidi ya nusu ya wachezaji wanaocheza katika kombe la dunia ndani ya kikosi Ivory Coast o wamelelwa katika kituo hicho cha michezo cha Asec, hali ambayo inatajwa kuwawezesha kucheza mpira wenye ustadi zaidi.
Baadhi ya wachezaji wa kimataifa kama Yaya Toure wamepitia katika taasisi hiyo
Hivyo siri kubwa na mafanikio ya soka nchini Ivory Coast ni pamoja na elimu ya kawaida ya darasani lakini bado vijana wamekuwa wakifanya bidii katika somo la kiingereza,Hesabu na kifaransa ,ambao wao wanasema masomo hayo ya lugha ni kwaajili ya kuwasaidia kwenda kuishi ulaya watakapokuwa wachezaji wa kimataifa.
Lakini pia utaratibu wa masomo nchini humo unawapa watoto fursa ya kushiriki michezo na kukuza vipaji vyao.
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment