Wanafunzi wa kitivo cha elimu katika chuo kikuu cha
Dodoma wameipindua serikali ya wanafunzi wa kitivo
hicho kwa madai ya kutowajibika kwa viongozi pamoja na
madai ya ubadhirifu wa fedha.
Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM).
Mapinduzi hayo yamefanyika leo asubuhi ambapo
wanafunzi hao wamempindua aliyekuwa Rais wa kitivo
hicho, John Nzilanyingi na kumuweka aliyekuwa waziri wa
afya na mikopo, Simon Mpandalume kuwa Rais wa mpito
wa serikali hiyo hadi hapo uchaguzi mkuu utakapofanyika
Juni mosi mwaka huu.
Rais aliyepinduliwa anadaiwa kutumia madaraka yake
vibaya kwa kuwakandamiza wanafunzi wenzake kwa
kushirikiana na uongozi wa chuo.
Aidha anatuhumiwa kwa ufujaji wa fedha za wanafunzi
ambapo anadaiwa kutumia sh milion 7 za michango ya
wanafunzi kununulia gari yake ya kutembelea.
Mpaka sasa Rais huyo hajulikani alipo kwani baada ya
kupinduliwa alitoweka eneo la chuo.
Monday, 1 June 2015
Wanachuo wapindua Serikali yao UDOM.
Related Posts:
Dkt Slaa atoa tathmini ya maamuzi anayofanya Rais Dkt Magufili.Aliyekuwa katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa ametoa tathmini yake kwa siku chache za Rais John Magufuli alizoanza kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano na maamuzi aliyoyafanya. Dkt. Slaa ambaye alikuwa mgombea u… Read More
Viti Maalum: BAWACHA Ruvuma wampa Mh. Mbowe siku 3.BAWACHA Mkoani Ruvuma wampa Mwenyekiti Mbowe siku tatu kutengua uamuzi wa kumteua Zubeda Sakuru Ubunge Viti Maalum, wasikitishwa na uteuzi huo wadai ni wa upendeleo-Aidha wameshangazwa na uongozi wa Chama kutotokea kwenye kik… Read More
Rais Dkt Magufuli apokea hati ya makabidhiano ya Ofisi ya Ikulu kutoka kwa Rais Mstaafu Dkt Kikwete leoPicha:-Rais Dk MagufuliJP akipokea hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu Dk J M. Kikwete Ikulu Dar leo. … Read More
Serikali yasimamisha wafanyakazi 4 kwa tuhuma za wizi wa kuaminika Kilimanjaro.Wafanyakazi wanne wa halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamesimamishwa kazi na mweka hazina wa hospitali ya machame amefukuzwa kazi kwa tuhuma mbili tofauti za wizi wa kuaminika wa kujipatia zaidi ya shs.74mil/=.… Read More
Bantuz MAGAZETINI-Soma kilichoandikwa katika Magazeti ya leo Novemba 13. BantuTz MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusoma na kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata ha… Read More
Mmmmh
ReplyDelete