Facebook

Monday, 26 May 2014

Tameka afunguka chanzo kilichomfanya aachane na Usher Raymond


ushertamek 

Aliyekuwa mke wa R&B superstar Usher, Tameka Raymond hivi karibuni ameweka wazi sababu ya ndoa yake kuvunjika na staa huyo na kusema ilisababishwa na matendo yake yaliyo mkera na kumsumbua Usher.
Tameka amesema kitendo cha kwenda nchini Brazil ilikufanya upasuaji wa Lipo kiliathiri akili yake na ndoa yake sana na kubadilisha jinsi Usher alivyokuwa akimchukulia mke wake.
Lipo au Liposuction ni upasuaji unaofanywa ilikutoa au kupunguza mafuta kwenye sehemu tofauti za mwili. Mara nyingi Lipo hufanywa tumboni ,makalio na kwenye mapaja.

Tameka alikuwa kwenye mahojiano yakutangaza kipindi chake cha uhalisia kilichoitwa Hollywood Exes Atlanta. Kipindi hichi kinahusu wanawake waliowahi kuwa kwenye ndoa na watu maarufu na baadae kuachana. Aliyekuwa mke wa mwigizaji Kevin Hart ‘Torrie’ na wanawake wengine watatu watahusika kwenye kipindi hicho.
Tameka alipewa kazi na Usher kama mbunifu wake mwaka 2006 na mwaka 2007 walivalishana pete za uchumba na harusi kufanyika. Ni familiya yenye watoto wakiume wawili.
Torrei aliyekuwa mke wa muigizaji Kevin amesema usaliti wa Kevin na mfanya biashara mwenzake Eniko ulipelekea ndoa yao kuvunjika.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata stor mbalimbali zinazowahusu wasanii

0 comments:

Post a Comment