Mchezaji kiungo cha kati wa
Argentina,Angel Di Maria ana shaka ikiwa atashiriki mechi ya nusu
fainali Jumatano ijayo kati ya Argentina na Uholanzi.
Hi ni baada ya mchezaji huyo kupata jeraha la Paja wakati wa mechi yao dhidi ya Ubelgiji ambapo walishinda bao moja bila.Kocha Alejandro Sabella alinukuliwa akisema: "Angel ana tatizo la Paja lake la kulia na kwamba atachunguzwa zaidi.
Di Maria aliingiza bao la ushindi katika mechi yao dhidi ya Switzerland katika awamu ya muondoano.
Enzo Perez wa Benfica alichukua nafasi yake katika mechi dhidi ya Ubelgiji.
0 comments:
Post a Comment