Muda wa saa tano wa kusimamisha mapigano kati ya Israel na Gaza umeanza, siku tisa baada ya mapigano kuzuka.
Waandishi wa habari wanasema, watu wamejipanga nje ya mabenki na foleni za magazi zimeanza kuonekana mitaani wakati watu wakijitokeza kwenda kutafuta mahitaji muhimu.
Mapigano yaliendelea hadi saa nne asubuhi ambapo muda wa kusimamisha mapigano ulipoanza.
Maafisa wa Gaza waansema mashambulio ya Israel yamesababisha vifo vya Wapalestina 227. Mashambulio ya roketi yaliyofanywa na Hamas yamesababisha kifo cha Muisraeli mmoja.
Israel ilianza harakati zake za kijeshi Julai 8 kwa lengo la kuzuia mashambulio ya roketi kutoka Palestina kwenda Israel.
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa unasema wengi wa waliouawa Gaza ni raia.
Israel inatuhumu Hamas kwa kuficha vifaa vya kijeshi miongoni mwa raia.
0 comments:
Post a Comment