
Kiungo wa Bayern Munich Toni Kroos amejiunga rasmi na Real Madrid kwa mkataba wa miaka sita kwa kitita ambacho hakikutajwa.
Kroos, 24, alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Ujerumani
kilichoishinda Argentina 1-0 kwenye fainali ya Kombe la Dunia nchini
Brazil.
Kiungo huyo atatambulishwa mbele ya mashabiki wa Real Madrid
kwenye dimba la Bernabeu siku ya Alhamisi, baada ya kukamilisha vipimo
vya afya.


0 comments:
Post a Comment