Gazeti moja la Uingereza limemuomba radhi mwigizaji nyota wa Marekani George Clooney, juu ya tuhuma ilizochapisha kuwa mama wa mchumba wake alikataa asifunge ndoa na mwanae kwa sababu za kidini.
Nyota huyo
wa Hollywood, Clooney, amemchumbia Amal Alamuddin- ambaye ni
mwanasheria- mwenye asili ya Lebanon, anayetoka katika jamii ndogo ya
Druse ambao ni Waislam.
Gazeti hilo, The Daily Mail liliripoti kuwa mama
wa mchumba wa Clooney alimtaka mwanaye huyo kuolewa na mtu kutoka jamii
ya Druse.
Gazeti hilo sasa limekiri kuwa taarifa hiyo si ya ukweli na
limeomba radhi kwa mtafaruku wowote uliotokana na habari hiyo.
0 comments:
Post a Comment