Facebook

Wednesday, 16 July 2014

Liverpool waanza vibaya mechi yao ya kwanza ya kirafiki.




Liverpool Leo hii huko Brondby, Denmark walichapwa Bao 2-1 katika Mechi yao ya kwanza ya Ziara yao ya kabla Msimu mpya kuanza walipofungwa na Wenyeji wao Club Brondby IF.
 
Wakiwa chini ya Meneja wao Brendan Rodgers ambae Msimu uliopita alifanya kazi kubwa kuisaidia kumaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Manchester City, Liverpool walichezesha Kikosi mchanganyiko na Kipindi cha Pili kilipoanza kubadili Wachezaji kumi.
Bao la kwanza la Brondby lilifungwa na Christian Norgaard kwenye Dakika ya 24.
 
Hadi Mapumziko Brondby 1 Liverpool 0.
Liverpool walisawazisha katika Dakika ya 48 kwa Bao la Kristoffer Peterson ambae aliingizwa kutoka Benchi.
Bao la ushindi kwa Brondby lilifungwa na Mchezaji wao kutoka Macedonia, Ferhan Hasani katika Dakika ya 90.
Hadi mwisho, Brondby 2 Liverpool 1.
 
Mechi inayofuata kwa Liverpool ni dhidi ya Preston Northend hapo Julai 19.
 
KIKOSI:
Liverpool:
Brad Jones, Kelly, Agger, Ilori, Smith, Lucas, Rossiter, Coutinho, Suso, Borini, Teixeira

Akiba: Ward, Allen, Ibe, Coady, Skrtel, Flanagan, Phillips, Wisdom, L. Jones, Peterson, Stewart

LIVERPOOL-ZIARA KABLA MSIMU:
16 Julai Brondby 2 Liverpool 1[Brondby, Denmark]
19 Julai Preston North End v Liverpool [Deepdale, Preston]
24 Julai Roma v Liverpool [Boston, USA]
28 Julai Liverpool v Club Olympiakos Nicosia

Related Posts:

  • Mourinho amtetea Van Gaal. Jose Mourinho amesema Meneja mpya wa Manchester United Louis van Gaal si Mtu wa kiburi ila ni mkweli. Mourinho, ambae sasa ni Meneja wa Chelsea, alifanya kazi chini ya Van Gaal huko Barcelona kati ya Mwaka 1997 n… Read More
  • Diaby apona baada ya majeraha ya muda mrefu.   Abou Diaby alifanikiwa kumaliza dakika 45 za kipindi cha pili jana wakati Arsenal wakianza mechi za maandalizi kwa ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Boreham Wood. Mara ya mwisho Diaby kuonekana dimbani ilikua March … Read More
  • FIFA yaiondolea kifungo Nigeria Shirikisho la soka duniani FIFA limendoa marufuku lililoiwekea Nigeria. Shirikisho hilo lilikuwa limeipiga marufuku Nigeria kutoshiriki katika michuano yoyote ya soka mapema mwezi huu kwa kuwa… Read More
  • "Van Persie Nahodha Mpya Man Utd"   "Manchester United imeondokewa na manahodha 3 kwa wakati mmoja(Vidic,Rio na Evra). Kwa sasa ni vigumu kupata nahodha atakayeishawishi klabu pamoja na wachezaji. Lakini Robin Van Persie anafaa kuwa nahodha wa M… Read More
  • Mfahamu kinda wa Arsenal anayeng'ara mechi za maandalizi ya msimu.   Huyu ndiye kinda Kristoffer Olsson, mfungaji wa bao la kwanza huku la pili likiwekwa nyavuni na kinda jingine Benik Afobe – kipindi cha pili kuhakikisha Arsenal wanaanza mwchi za maandalizi kwa ushindi. Arsene… Read More

0 comments:

Post a Comment