Kupenda ama kutamani kuwa kama star fulani unaemkubali hakuna sheria ya
mipaka zaidi ya mwenyewe kuthibiti hisia zako zisipitilize, lakini wapo
wengine ambao wamechoka kutamani kuwa kama fulani na wameamua kutumia
nguvu kuwa kama yeye.
Claire Leeson, msichana mwenye umri wa miaka 24, mkaazi wa Landani
ametumia zaidi ya $30,000 (Tsh 49,755000)kufanya upasuaji ili afanane na
Kim Kardashian.
Claire ameiambia This Morning kuwa aliamua kufanya hivyo kwa sababu
alipokuwa shuleni wenzake walikuwa wanamcheka na kuuita ‘mbaya’ kuliko
kitu chochote kilicho hai.
“Nilikuwa naambiwa kila siku mimi ndiye mbaya kuliko kitu chochote
kilicho hai na kwamba inabidi nijiue. Nilipoacha shule marafiki zangu
waliniambia kuwa ninavitu ambavyo vinafanana na Kim Kardashian.” Amesema Claire.
Ameeleza kuwa baada ya kuambiwa hivyo na marafiki zake aliamua kuanza
kuangalia kwa makini Keeping Up With The Kardashians na akagundua kuwa
kweli kuna vitu ambavyo wanafanana na Kim Kardashian.
“Tunafanana katika mabishano na vitu vingine. Nikafikiri ni mzuri sana na kwa kweli nilitaka kufanana nae.”
0 comments:
Post a Comment