MAHARI YAZIDI KULETA KASHESHE INDIA
Mahakama kuu ya India imesema wanawake wanazidi kutumia vibaya sheria zinazokataza malipo ya mahari kwa kuwanyanyasa waume na wakwe zao.
Mahakama kuu ya India imesema wanawake wanazidi kutumia vibaya sheria zinazokataza malipo ya mahari kwa kuwanyanyasa waume na wakwe zao.
Iwapo
mwanamke atashtaki kuwa mume wake au ndugu wametaka mahari, hukamatwa
mara moja. Lakini wanaume wengi waliokamatwa wamekutwa hawana hatia.
Tofauti na sehemu nyingi duniani wanawake ndio hutoa mahari nchini India
wanapoolewa. Mahakama sasa imeamrisha polisi kukusanya ushahidi kwanza
kabla ya kukamata mtu yeyote kuhusiana na masuala ya mahari.
Utoaji
mahari ulipigwa marufuku zaidi ya miaka hamsini iliyopita lakini
unaendelea kushamiri na wanaharakati wanasema husababisha wanawake
kunyanyaswa na hata kuuawa.
0 comments:
Post a Comment