Facebook

Thursday, 10 July 2014

Mananchester United waanza mazoezi, wa"Mkopo" wote warejea.

MANCHESTER UNITED walianza Mazoezi rasmi kwa ajili ya Ziara ya Kabla Msimu Mpya ya huko Marekani na Wachezaji kadhaa waliokuwa nje kwa Mkopo Msimu uliopita wamerejea na kujumuika huko AON Training Complex Jijini Manchester
Kutokuwepo kwa Meneja mpya, Louis van Gaal, ambae bado yuko Brazil akiiongoza Netherlands kwenye Kombe la Dunia, kulikifanya Kikosi hicho kuwa chini ya Meneja Msaidizi Ryan Giggs.
Wachezaji hao walianza kurudi Klabuni tangu Ijumaa iliyokwisha kwa ajili ya upimwaji Afya zao na Mazoezi rasmi kupangwa kuanza mapema wiki hii.
Miongoni mwa Wachezaji wa Timu ya Kwanza waliokuwepo hiyo ni pamoja na Mchezaji mpya Ander Herrera na kina Jonny Evans, Michael Carrick, Darren Fletcher, Tom Cleverley na Rafael Da Silva.
Lakini pia Wachezaji kadhaa waliokuwa nje kwa Mkopo Msimu uliopita walirejea na hao ni kina Bebe, Anderson,
Wilfried Zaha, Angelo Henriquez, Jesse Lingard na Nick Powell.
Bebe alikuwa huko kwao Ureno na Klabu ya Paços de Ferreira, Anderson alikuwa Italy na Fiorentina huku Angelo Henriquez, Mchezaji kutoka Chile, alichezea Real Zaragoza.
Msimu uliopita Wilfried Zaha alikuwa Cardiff City, Jesse Lingard alikuwepo Brighton na Nick Powell kuichezea Wigan Athletics.
Wiki hii, Ryan Giggs anatarajiwa kukutana na kila Mchezaji na kuongea nao ana kwa ana.
Wachezaji wengine ambao wamechelewa kujiunga na wenzao ni wale waliokuwepo huko Brazil na Timu zao za Taifa kwenye Fainali za Kombe la Dunia lakini baadhi yao wanatarajiwa wote kuwepo kwenye Ziara ya Mareakani.
Hao ni pamoja na Shinji Kagawa, aliekuwa na Japan huko Brazil, David De Gea, aliekuwa na Spain na Wachezaji wa England ambao ni Wayne Rooney, Chris Smalling, Phil Jones, Danny Welbeck na Mchezaji mpya Luke Shaw.
Man United wataruka hapo Julai 18 kuelekea huko Marekani na kupiga Kambi huko California kabla ya kucheza Mechi yao ya Kwanza huko USA hapo Julai 23 dhidi ya LA Galaxy kugombea Chevrolet Cup ndani ya Rose Bowl, Pasadena.
 MAN UNITED WAANZA MAZOEZI, WA ‘MKOPO’ BEBE, ANDERSON, ZAHA….WAREJEA!
Tuesday, 08 July 2014 19:48

MANCHESTER UNITED Jana walianza Mazoezi rasmi kwa ajili ya Ziara ya Kabla Msimu Mpya ya huko Marekani na Wachezaji kadhaa waliokuwa nje kwa Mkopo Msimu uliopita wamerejea na kujumuika huko AON Training Complex Jijini Manchester

Kutokuwepo kwa Meneja mpya, Louis van Gaal, ambae bado yuko Brazil akiiongoza Netherlands kwenye Kombe la Dunia, kulikifanya Kikosi hicho kuwa chini ya Meneja Msaidizi Ryan Giggs.

Wachezaji hao walianza kurudi Klabuni tangu Ijumaa iliyokwisha kwa ajili ya upimwaji Afya zao na Mazoezi rasmi kupangwa kuanza Jana Jumatatu.

Miongoni mwa Wachezaji wa Timu ya Kwanza waliokuwepo hiyo Jana ni pamoja na Mchezaji mpya Ander Herrera na kina Jonny Evans, Michael Carrick, Darren Fletcher, Tom Cleverley na Rafael Da Silva.

Lakini pia Wachezaji kadhaa waliokuwa nje kwa Mkopo Msimu uliopita walirejea na hao ni kina Bebe, Anderson,

Wilfried Zaha, Angelo Henriquez, Jesse Lingard na Nick Powell.

Bebe alikuwa huko kwao Ureno na Klabu ya Paços de Ferreira, Anderson alikuwa Italy na Fiorentina huku Angelo Henriquez, Mchezaji kutoka Chile, alichezea Real Zaragoza.

Msimu uliopita Wilfried Zaha alikuwa Cardiff City, Jesse Lingard alikuwepo Brighton na Nick Powell kuichezea Wigan Athletics.

Wiki hii, Ryan Giggs anatarajiwa kukutana na kila Mchezaji na kuongea nao ana kwa ana.

Wachezaji wengine ambao wamechelewa kujiunga wenzao ni wale waliokuwepo huko Brazil na Timu zao za Taifa kwenye Fainali za Kombe la Dunia lakini baadhi yao wanatarajiwa wote kuwepo kwenye Ziara ya Mareakani.

Hao ni pamoja na Shinji Kagawa, aliekuwa na Japan huko Brazil, David De Gea, aliekuwa na Spain na Wachezaji wa England ambao ni Wayne Rooney, Chris Smalling, Phil Jones, Danny Welbeck na Mchezaji mpya Luke Shaw.

Man United wataruka hapo Julai 18 kuelekea huko Marekani na kupiga Kambi huko California kabla ya kucheza Mechi yao ya Kwanza huko USA hapo Julai 23 dhidi ya LA Galaxy kugombea Chevrolet Cup ndani ya Rose Bowl, Pasadena.

USA-ZIARA YA KABLA MSIMU MPYA:

[Zote Nchini Marekani]

Manchester United v LA Galaxy

Chevrolet FC Cup

Jumatano 23 Julai 2014, Rose Bowl, Pasadena

Manchester United v AS Roma

International Champions Cup

Jumamosi 26 Julai 2014, Sports Authority Field, Denver

Manchester United v Inter Milan

International Champions Cup

Jumanne 29 Julai 2014, FedEx Field, Washington DC

Manchester United v Real Madrid

International Champions Cup

Jumamosi 2 Agosti 2014, Michigan Stadium, Ann Arbor

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment