Facebook

Sunday, 6 July 2014

Marekani yachukizwa na hatua ya Israel

Ghasia kati ya Palestina na Israel
Marekani imesema kuwa ina wasiwasi mwingi kwamba maafisa wa Polisi wa Israel wamempiga vibaya kijana mmoja raia wa Marekani.
Idara ya maswala ya kigeni imesema kuwa inashtumu utumiji wa nguvu kupitia kiasi na kutaka uchunguzi wa haraka na ulio huru kufanywa .
Kijana huyo Tariq Khdeir ni binamu wa Mohammed Abu Khdeir ,kijana wa kipalestina ambaye mauaji yake mashariki mwa Jerusalem yamezua ghasia.
Polisi ya Israel inasema kuwa kijana huyo ni miongoni mwa raia sita wa kipalestina waliojihami ambao walikamatwa wakati wa ghasia hizo.
lakini baba ya kijana huyo anasema mwanawe hakuhusika kamwe.
Ghasia hizo zilienea hadi katika miji mingine ya kiarabu nchini Israel siku ya jumamosi kufuatia ripoti kwamba Mohammed Abu Khdeir alichomwa akiwa mzima.

Related Posts:

  • Sudan kusini yakabiliwa na baa la njaa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini kama mbaya zaidi kuwahi kuonekana duniani na kuyataka mataifa ambayo yaliahidi kutoa msaada wa zaidi ya dola millioni mia sita ku… Read More
  • Ebola yakaribia Nigeria Madaktari wanaokabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone Serikali ya Nigeria imesema kuwa imeweka hali ya tahadhari katika maeneo yote ya kuingia… Read More
  • Sudan kusini yakabiliwa na baa la njaa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini kama mbaya zaidi kuwahi kuonekana duniani na kuyataka mataifa ambayo yaliahidi kutoa msaada wa zaidi ya dola millioni mia sita ku… Read More
  • Gaza:Makubaliano ya saa 12 yaheshimiwa Kiongozi wa Hamas na mwenzake wa Israel Serikali ya Israel na wapiganaji wa Hamas wameanza kutekeleza makubaliano ya kusitisha vita kwa masaa 12 katika … Read More
  • Mgonjwa wa Ebola asakwa Sierra Leone Mamlaka nchini Sierra Leone inataka usaidizi kutoka kwa raia wake ili kumsaka mgonjwa mmoja wa Ebola ambaye alichukuliwa kwa lazima na … Read More

0 comments:

Post a Comment